Kilimo Biashara | Tunaangazia kilimo cha mafenesi katika kaunti ya Busia
Wakulima katika maeneo ya magharibi ya Kenya wameanza harakati za kufufua kilimo cha fenesi, katika hatua ya kukuza upya tunda hilo la jadi. Hii ni kutokana na umaarufu wa matunda haya, ambayo sasa wakaazi huyaagiza kutoka taifa jirani la Uganda.