Kinara wa Azimio asisitiza maandamano kuendelea kesho
Kinara wa Azimio Raila Odinga ameshikilia kuwa maandamano dhidi ya serikali yataendelea hapo kesho kama yalivyopangwa. Odinga akisisitiza kuwa maandamano hayo yatafanyika siku mbili kama alivyotangaza. Na kama Laura Otieno anavyoarifu, Gavana wa Kisumu Anyang Nyong'o amebatilisha agizo lake la kupiga marufuku maandamano ya hapo kesho Kisumu, na kutangaza kuwa pia yataendelea.