Rais Ruto afanya uteuzi kwenye mashirika mbalimbali huku wandani wa Uhuru wakipigwa kalamu
Rais William Ruto amefanya uteuzi mbalimbali katika mashirika ya serikali. Kupitia gazeti rasmi la serikali, rais ruto amewapa kazi aliyekuwa gavana wa pokot magharibi John Lonyangapuo, aliyekuwa waziri wa maswala ya afrika mashariki na katibu wa biashara na utalii John Konchella miongoni mwa wengine.