Kutana na Gari Kubwa Kuliko Yote Duniani (Linatembea)

Ukweli ni kuwa bado kuna mambo mengi sana ya kushangaza hasa upande wa teknolojia na uwandisi, Kama unakumbuka tulisha wahi kuangalia gari lenye uwezo wa kupaa na kutembea kwenye barabara, lakini leo ni vyema tuangalie Gari kubwa kuliko yote na pia lenye uwezo wa kutembea.Gari hili ndani yake lina vyumba vya kulala, sebule kubwa, jiko pamoja na sehemu nyingine za kukaa. Yaani unaweza kusema uko ndani ya meli.Gari hii inaitwa Hummer H1 X3, gari hii imetengezwa kuwa muda wa mwaka mmoja na nusu na gari hili linamilikiwa na Sheikh Hamad, ambae pia hujulikana kwa jina la “Rainbow Sheikh”. Gurudumu moja la gari hili lina thamani ya dollar za marekani $25,000 ambayo ni sawa na takribani Milioni 63 za Tanzania.Kuingia kwenye gari hili unatumia gazi maalum ambayo ipo chini ya gari hilo na unapo ingia tu kwenye gari hilo chumba cha kwanza ni jiko, pamoja na sehemu ya maliwato.Gari hii pia inatumia Engine, nne ambazo ziko kwenye kila upande wenye gurudumu. Yaani kila gurudumu linaendeshwa na Engine yake pekee.Gari hili pia lina ghorofa mbili, ghorofa ya juu ndio ambapo kuna sehemu ya kulala, pamoja na sehemu ya kupumzika ambayo pengine ni kubwa kuliko seble ya nyumba ya kupanga ya TZS 500,000 hapa dar es salaam.Muendeshaji wa gari hili kubwa kuliko yote yeye anakaa nyuma na sidhani kama ni rahisi kuendesha gari hili kutokana na muonekano wa sehemu yake ya usukani. Mbali na hayo kila Engine ya gari hili huwashwa kivyake na kuongozwa kivyake.Gari hili ni moja ya magari ya ajabu ambayo yana milikiwa na Sheikh Hamad, au “Rainbow Sheikh” ambaye anasemekana kumiliki magari zaidi ya 3000 yenye sura na uwezo tofauti. Sheikh Hamad anao utajiri unaokadiriwa kufikia dollar za marekani Bilioni 20, sawa na takribani Trilioni 50 za Kitanzania.Kwa sasa tajiri huyo ametengenza sehemu maalumu za maonyesho ambazo, ameweka magari zaidi ya 200 yenye muonekano wa tofauti. Baadhi ya magari hayo yame tengenezwa maalum kwaajli yake hivyo hutoweza kuyaona sehemu nyingine yoyote.Oh! na kama unajiuliza kwa nini Sheikh huyu anaitwa Rainbow Sheikh, hii ni kwa sababu anamiliki magari ya aina ya Mercedes-Benz yenye rangi zote mbalimbali ambazo ziko kwenye Rainbow.

Dec 3, 2023 - 17:35
 0
Kutana na Gari Kubwa Kuliko Yote Duniani (Linatembea)
Ukweli ni kuwa bado kuna mambo mengi sana ya kushangaza hasa upande wa teknolojia na uwandisi, Kama unakumbuka tulisha wahi kuangalia gari lenye uwezo wa kupaa na kutembea kwenye barabara, lakini leo ni vyema tuangalie Gari kubwa kuliko yote na pia lenye uwezo wa kutembea.Gari hili ndani yake lina vyumba vya kulala, sebule kubwa, jiko pamoja na sehemu nyingine za kukaa. Yaani unaweza kusema uko ndani ya meli.Gari hii inaitwa Hummer H1 X3, gari hii imetengezwa kuwa muda wa mwaka mmoja na nusu na gari hili linamilikiwa na Sheikh Hamad, ambae pia hujulikana kwa jina la “Rainbow Sheikh”. Gurudumu moja...

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow