Maujanja ya WhatsApp Hambayo Ulikuwa Hujui (2023)

WhatsApp imepata mabadiliko makubwa mwaka wa 2023, ikiongeza vipengele vingi vipya ikiwa pamoja na kubadilisha muonekano wake. Licha ya sasisho hizi, watumiaji wengi bado hawajui vipengele muhimu vinavyopatikana kwenye programu ya WhatsaApp kupitia makala hii, tutaangalia vipengele bora vipya vya WhatsApp na jinsi vinavyoweza kuboresha na kuleta urahisi wakati unatumia programu ya WhatsApp.Ujumbe wa VideoWakati ujumbe wa sauti “Voice Note” unatumiwa sana na watumiaji wa App ya WhatsApp, lakini unajua kuwa unaweza pia kutuma ujumbe wa video?. Kwa kuwezesha kipengele cha ujumbe wa video wa papo hapo katika settings ya WhatsApp, unaweza kubadilisha kwa urahisi kutoka kutuma ujumbe wa sauti hadi ujumbe wa video. Ujumbe huu unaweza kuplay bila usumbufu ndani ya meseji zako kwa inavyokuwa ujumbe wa sauti “Voice Note”.Kuwasha sehemu hii ingia kwenye sehemu ya Settings > Chats > Instant Video Messages, kisha washa sehemu hii na moja kwa moja utakuwa na uwezo wa kutumia ujumbe wa video.Hariri Ujumbe uliotumwaJe, umewahi kutuma meseji ya WhatsApp yenye ujumbe wenye maelezo yasiyo sahihi? Kupitia uwezo wa kuhariri ujumbe uliotumwa, sasa kupitia app ya WhatsApp unaweza kurekebisha haraka makosa yoyote. Bonyeza tu na ushikilie ujumbe uliotumwa, chagua chaguo la kuhariri, na ufanye mabadiliko muhimu.Hata hivyo ujumbe uliohaririwa unawekwa alama maalum ya kuonyesha ujumbe umehaririwa, hata hivyo una dakika 15 za kuhariri ujumbe baada ya kuutuma.Funga na Ficha Meseji za WhatsAppIkiwa unathamini faragha katika mazungumzo yako ya WhatsApp, kipengele cha kufunga na kuficha meseji ni muhimu kwako. Kwa kuwezesha kipengele hiki, unaweza kuficha na kufunga meseji kwa kutumia alama ya kidole chako au utambulisho wa uso.Kuficha meseji za mtu unaechat nae ingia kwenye chat kisha bofya profile ya mtu unaechat nae kisha tafuta kipengele cha Chat Lock, kisha weka ulinzi kati ya ulinzi wa uso, au fingerprint.Meseji zilizofungwa zinafichwa kwajuu ya screen kwenye uwanja wa meseji za WhatsApp na unaweza kuzipata kwa kuvuta chini kwenye sehemu uwanja wa meseji zote au Chats.Ingia WhatsApp kwa Barua pepeWhatsApp sasa imeleta uwezo wa kuthibitisha na kuingia kwenye akaunti yako ya WhatsApp kwa barua pepe. Kwa kuongeza anwani yako ya barua pepe katika mipangilio ya akaunti, unaweza kupokea OTP (nambari za siri za muda) kupitia barua pepe ikiwa nambari yako ya simu haifanyi kazi. Kipengele hiki kinahakikisha kuwa bado unaweza kuingia katika akaunti yako ya WhatsApp hata ukikumbana na matatizo na nambari yako ya simu. Ni muhimu kuzingatia kwamba anwani yako ya barua pepe inabaki kuwa ya faragha na haiwezi kuonekana na mtu yeyote kwenye WhatsApp.Ubora wa Picha na VideoLinapokuja suala la kushiriki au kushare picha na video, mifumo ya WhatsApp mara nyingi imekuwa ikiharibu ubora wa faili za media kwa kuconvert picha na video kabla ya kutuma.Hata hivyo, sasisho la hivi karibuni limeleta chaguo la HD kwa kutuma picha na video za ubora wa juu. Sasa unaweza kuchagua kutuma picha au video zenye ubora wa kati yaani (SD) na picha na video zenye ubora wa juu yaani (HD).Jinsi ya kutuma picha za ubora wa juu HD au ubora wa kati SD, unatakiwa kuchagua sehemu ya HD kabla ya kutuma, na utaletewa sehemu ya kuchagua kati ya HD ua SD.Mabadiliko ya Sehemu ya StatusHivi karibuni WhatsApp imeboresha kipengele cha Status. Sehemu hii sasa inakuja na sehemu mpya ya kushare link zenye muonekano bora kwenye Status, pamoja na hayo pia utaweza kutuma meseji za sauti kwenye Status.Ili Kutuma meseji za sauti ingia kwenye sehemu ya Status, kisha moja kwa moja bofya kitufe cha kalamu na chagua text alafung utaona sehemu ya ujumbe wa sauti bofya na shikilia kurekodi ujumbe wako kwa ajili ya kuweka kwenye Status.Akaunti Mbili za WhatsApp Kwenye Simu MojaKama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kutumia namba mbili tofauti za whatsapp kwenye simu yako moja sasa inawezekana, kupitia sehemu hii utaweza kuongeza namba nyingine ya WhatsApp ambao zote zitakuwa zinatumika kwenye simu moja.Unachotakiwa kufanya ni kubofya na shikilia kidogo profile picha yako kwenye app ya WhatsApp na moja kwa moja utaletewa sehemu ya kuongeza akaunti. Kwa kufanya hivyo utaweza kuswitch kati ya namba moja na nyingine kwa kubofya kwa muda kwenye sehemu ya kubadilisha akaunti kama inavyokuwa kwenye Instagram. Sehemu hii inapatikana kwenye WhatsApp ya kawaida na sio WhatsApp Business.Sehemu Mpya ya WhatsApp ChannelKama wewe ni mmoja wa watumiaji mahiti wa programu ya WhatsApp ni muhimu sana kufahamu sehemu ya WhatsApp channel. Sehemu hii ni muhimu hasa kwa wafanya biashara na watu wote wanaopenda kutoa taarifa kuhusu bidhaa au huduma yoyote.Kupitia sehemu ya WhatsApp Channel unaweza ku-post link, video na maandishi mbalimbali kupitia Channel yako. Kwa sasa WhatsApp tayari inaruhusu watumiaji wote kutengeneza channel na unaweza kutengeneza channel yako kupitia sehemu ya Updates > kisha bofya kitufe cha jumlisha kuongeza channel yako.Kama unataka kupata maujanja na habari mpya kwa haraka unaweza kujiunga n

Dec 3, 2023 - 17:35
 0
Maujanja ya WhatsApp Hambayo Ulikuwa Hujui (2023)
WhatsApp imepata mabadiliko makubwa mwaka wa 2023, ikiongeza vipengele vingi vipya ikiwa pamoja na kubadilisha muonekano wake. Licha ya sasisho hizi, watumiaji wengi bado hawajui vipengele muhimu vinavyopatikana kwenye programu ya WhatsaApp kupitia makala hii, tutaangalia vipengele bora vipya vya WhatsApp na jinsi vinavyoweza kuboresha na kuleta urahisi wakati unatumia programu ya WhatsApp.Ujumbe wa VideoWakati ujumbe wa sauti “Voice Note” unatumiwa sana na watumiaji wa App ya WhatsApp, lakini unajua kuwa unaweza pia kutuma ujumbe wa video?. Kwa kuwezesha kipengele cha ujumbe wa video wa papo hapo katika settings ya WhatsApp, unaweza kubadilisha kwa urahisi kutoka kutuma ujumbe wa sauti...

What's Your Reaction?

like

dislike

love

funny

angry

sad

wow