Tamasha la Chaka Tu Chaku litakuwa mwokozi kwa wasanii Ta
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amelizungumzia Tamasha lililokuja kwa namna ya kipekee linaloitwa CHAKA TU CHAKA ambalo limeonekanna likipigiwa debe na wachekeshaji Mkojani na Tine White. Wengi wameliona Tamasha hili baada ya video ya Rich Mavoko ku-trend akionekana akifanya show vijijini na watu kuhoji imekuwaje Mavoko kufanya show kama zile vijijini kutokana na ukubwa wake?? Jibu ni kwamba wasanii wengi Tanzania hawapati show kubwa ambazo zimeandaliwa na wasannii wenzao au taasisi mbalimbali na wao wanahitaji pesa z akuendeshea maisha yao. Kama Tamasha hili litakuwa na mwendelezo mzuri linaweza kuwa na faid akubwa sana kwa baadhi ya wasanii ambao hawapati nafasi ya kuburudisha mashabiki wao katika ameneo mbalimbali. Kutokana na sehemu wanazoenda linaweza kujipatia umaarufu mkubwa na siku zijazo kuja kuwa moja ya Matamsha makubwa sana nchini kwa sababu litakuwa linagusa wasanii wa kila aina. Licha ya kuwa wasanii wanahitaji kupata pesa lakini pia mashabiki wa vijijini wamekuwa kama wametengwa, hawafikiwi na matamasha makubwa hivyo Tamasha hili litakuwa fursa kwao maana hata wao wana haki ya kuburudishwa na wasanii wao wanaowapenda. Uzuri wake Mkojani na Tine White wamesema wapo tayari kuleta wasanii wa kimataifa na kuwapeleka vijijini hivyo itakuwa fursa nzuri sana.

What's Your Reaction?






